Papa atoa salamu za Pasaka kwa Wakatoliki
20 Aprili 2025Matangazo
Papa Francis mwenye umri wa miaka 88 amekuwa akiuguwa kwa muda na hali yake ni dhaifu hivyo basi ameshindwa kuonekana kwa matukio mengi muhimu ya kiroho katika wiki nzima hii ya sikukuu hiyo muhimu katika kalenda ya Ukristo, ikiwemo Jumapili ya Pasaka. Kawaida kiongozi huyo wa kiroho wa kanisa katoliki duniani hutowa hotuba yake ya kiroho na baraka kwa waumini akiwa kwenye roshani akiwatazama waumini kwenye uwanja huo wa kanisa la mtakatifu Peter baada ya ibada ya maadhimisho ya siku ya Pasaka. Kutokana na afya yake iliyodhoofika kutokana na homa ya mapafu haikufahamika ikiwa kiongozi huyo atashiriki kwenye tukio hilo la ibada na kwa kiwango gani.