SiasaPanama
Panama yampa siku tatu rais wa zamani kwenda uhamishoni
1 Aprili 2025Matangazo
Martinelli amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 10 jela kwa hatia ya utakatishaji fedha nchini mwake.
Tamko la serikali ya Panama, ambalo limempa rais huyo wa zamani siku tatu zaidi za kuondoka, linafuatia lile la serikali ya Nicaragua, ambayo hapo jana ilisema isingelimruhusu kuingia hadi Panama iweke wazi endapo imeomba waranti ya polisi ya kimataifal, Interpol, dhidi ya kiongozi huyo.
Ruhusa hiyo ya serikali ya Panama inakuja ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu Martinelli kuomba hifadhi kwenye ubalozi wa Nicaragua.