Pakistan yapewa siku 10 kurejesha katiba
13 Novemba 2007Matangazo
Bhutto,kwa mara nyingine tena amewekwa katika kizuizi cha nyumbani katika mji wa mashariki wa Lahore.Serikali imesema,hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu ya kuwepo vitisho vya kutaka kumuua.Lakini chama cha Bhutto cha Pakistan People´s Party kinasema,azma ni kumzuia kuongoza maandamano ya kupinga hali ya hatari iliyotangazwa na Rais Pervez Musharraf Novemba 3.
Kwa upande mwingine,Jumuiya ya Madola imeipa Pakistan muda wa siku 10 kurejesha katiba ya nchi na kuondosha hali ya hatari.Isipofanya hivyo itafukuzwa kutoka Jumuiya ya Madola.