MigogoroAsia
Pakistan yaionya India dhidi ya kurudia kuishambulia
13 Mei 2025Matangazo
Serikali mjini Islamabad imeiyataja matamshi hayo ya Modi aloyatoa jana Jumatatu kuwa "ya kichokozi" na kuapa kuwa mashambulizi yoyote ya India yatajibiwa kwa nguvu zote na Pakistan.
Modi aliionya jana kuwa India iyatashambulia maficho yote ya magaidi kwenye eneo la mpaka wa nchi hizo mbili iwapo kutatokea hujuma nyingine dhidi ya India.
Hayo yalikuwa matamshi ya kwanza ya Modi hadharani tangu nchi hizo mbili jirani zilipotumbukia kwenye makabiliano ya kijeshi baada ya India kuituhumu Pakistan kuhusika na shambulizi la kigaidi katika jimbo linalozozaniwa la Kashmir.
Shambulizi hilo la Aprili 22 lilisababisha vifo vya watu 26.