SiasaPakistan
Pakistan yafanya majaribio ya kombora la masafa marefu
4 Mei 2025Matangazo
Mvutano uliosababishwa na shambulizi liliyofanyika kwenye jimbo la mgogoro la Kashmir mwezi uliopita. Jeshi la Pakistan limesema kombora hilo linaweza kurushwa hadi umbali wa kilometa 450.
Mpaka sasa India haijatoa kauli yoyote juu ya majaribio hayo. India inailaumu Pakistan kwa mauaji yalilofanywa hivi karibuni kwenye mji wa mapunziko wa Pahalgam.
Hata hivyo Pakistan imekanusha tuhuma hizo. Rais wa Pakistan, Asif Ali Zardari na waziri wake mkuu wamewapongeza waliyoyafanikisha majaribio ya kombora hilo.