MigogoroAsia
Pakistan yadungua droni 25 za India na kuahidi kulipa kisasi
8 Mei 2025Matangazo
Pakistan pia imeripoti kuzidungua karibu droni 25 za India. Mamlaka ya usafiri wa anga ya Pakistan imetangaza kuwa viwanja vya ndege katika miji mikuu mitatu ya Karachi, Lahore na Islamabad vitafungwa hadi saa kumi na mbili jioni.
Baraza la usalama linalowajumuisha mawaziri kadhaa wa Pakistan limetoa ruhsa kwa jeshi la nchi hiyo kulipa kisasi mashambulizi ya India.
Waziri wa Mambo ya Nje wa India Subrahmanyam Jaishankar ameonya kuwa watajibu vikali mashambulizi yoyote ya Pakistan, na hivyo kuzusha wasiwasi katika eneo la Asia Kusini, huku juhudi za kidiplomasia za kutuliza mzozo huo zikiendelea.