MigogoroAsia
Pakistan yadai kuwa India inajiandaa kuishambulia
30 Aprili 2025Matangazo
Attaullah Tarar ameapa kwamba shambulio lolote la India litajibiwa vikali, huku kukiwa na wasiwasi wa kushuhudia kuongezeka kwa mzozo huo baina ya mataifa hayo mawili- yenye kumiliki silaha za nyuklia.
Soma pia: Wanajeshi wa Pakistan na India washambuliana huko Kashmir
Kauli ya serikali ya Pakistan imetolewa baada ya hapo jana Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kufanya mkutano wa faragha na maafisa wakuu wa jeshi na polisi na kuwapa wanajeshi kile alichokitaja kuwa "uhuru kamili wa kufanya kazi" ili kujibu shambulio la wiki iliyopita huko Pahalgam katika eneo linalozozaniwa la Kashmir.