Pakistan kuchukua urais wa Baraza la Usalama
1 Julai 2025Matangazo
Pakistanleo inatarajiwa kuchukua urais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa mwezi wa Julai. Vyombo vya habari nchini India vinasema serikali mjini New Delhi ina mkakati wa kuukabili msimamo wa sasa wa Pakistan.
Pakistan ilianza muhula wake wa miaka miwili kama nchi mwanachama wa Baraza la Usalama isiyo na kiti cha kudumu mnamo Januari mwaka huu.
Huu ni urais wake wa kwanza tangu mwaka 2013 na ni mara ya nane kwa nchi hiyo kuhudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.