Pakistan inapanga kumpeleka Marekani gaidi mtuhumiwa Faradj El Libbi wa kutoka Libya
1 Juni 2005Matangazo
Islamabad:
Pakistan inapanga kumpeleka Marekani,gaidi mtuhumiwa Abu Faradj el Libbi aliyekamatwa mapema mwezi uliopita.Rais Pervez Musharraf,amekiambia kituo cha matangazo cha CNN,watumishi wa idara ya usalama wamegundua nyara kadhaa wanazozihitaji.Raia huyo wa Libya anatajikana kua dhamana wa ngazi ya juu,watatu nyuma ya kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa Al Qaida,.Ossama Ben Laden.Ofisi ya mwanasheria mkuu nchini Pakistan inamtuhumu Abu Farradj el Libbi kua nyuma ya mashambulio mawili yaliyofanywa mwaka 2003 dhidi ya rais Musharraf.Marekani imetenga kitita cha Dala milioni 10 kwa yeyote atakaewakabidhi El Libbi.