OFISI ZA AL-ARABIYA ZAFUNGWA IRAQ
25 Novemba 2003BAGHDAD: Polisi nchini Iraq wamezifunga ofisi za stesheni ya televisheni Al-Arabiya.Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kituo hicho cha matangazo ya Kiarabu kwa njia ya satalaiti,kutangaza kanda ya sauti inayosemekana kuwa ni ya rais mpinduliwa Saddam Hussein.Kanda hiyo inatoa muito wa kuwaua wajumbe wa Baraza Tawala la Wairaqi.Baraza hilo lililochaguliwa na Marekani,limetangaza kuwa linachukua hatua ya kisheria dhidi ya Al-Arabiya kuambatana na sheria mpya inayovizuia vyombo vya habari kuchochea chuki.Vile vile limetishia kuvifunga vituo vya CNN na BBC.Makundi yanayopigania haki za vyombo vya habari,yakiwa na makao yake katika nchi za magharibi,yamelaani vipingamizi hivyo.Makundi hayo yamesema vizuizi hivyo vinakiuka uhuru wa vyombo vya habari.