Nyota wa Liverpool Diogo Jota afariki katika ajali
3 Julai 2025Matangazo
Ajali hiyo ilitokea karibu na mji wa kaskazini-magharibi mwa Uhispania wa Zamora. Risala za rambirambi zinaendelea kumiminika kutoka kila pembe ya dunia zikiomboleza kumpoteza mchezaji mwenye hadhi , talanta na aliyekuwa hodari wa kufunga mabao.
Ajali hii imetokea siku chache tu baada Diogo Jota aliyekuwa na umri wa miaka 28 kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu Rute Cardoso.