Nigeria yapokea chanjo za ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo
5 Aprili 2025Matangazo
Katika taarifa yake, UNICEF imesema kuwa mripuko huo tayari umewaua zaidi ya watu 70 na kuambukiza zaidi ya wengine 800 katika majimbo 23 kati ya 36 ya nchi hiyo.
Waziri wa Afya wa Nigeria, Muhammad Ali Pate, amesema kuwasili kwa dozi za chanjo hiyo ya Men5CV ni hatua muhimu katika kampeni ya nchi hiyo kupambana na mripuko huo.
KAMPALA: Homa ya uti wa mgongo imesababisha vifo Uganda
Nigeria, taifa lenye wakaazi milioni 220, ni mojawapo ya nchi 26 za bara Afrika zinazokabiliwa na hatari kubwa ya maambukizi ya ugonjwa wa homa ya uti wa mgongo, katika eneo linalojulikana kama Ukanda wa Afrika wa ugonjwa huo unaoanzia Senegal katika eneo la magharibi hadi Ethiopia katika eneo la mashariki.