Nigeria yaomboleza kifo cha Muhammadu Buhari
14 Julai 2025Matangazo
Taarifa iliyotolewa na rais wa sasa wa nchi hiyo Bola Tinubu imesema kiongozi hiyo amemtuma makamu wake Kashim Shettima kwenda mjini London kuratibu maandalizi na kuusindikiza mwili wa Buhari kurejea Nigeria. Rais Tinibu amesema mtangulizi wake aliaga dunia kutokana na ugonjwa wa muda mrefu ambao hakuutaja.
Viongozi kadhaa wa Afrika akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf wametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Buhari.
Buhari aliitawala Nigeria mara mbili akiwa kwanza mtawala wa kijeshi mnamo miaka ya 1980 na mnamo mwaka 2015 alichaguliwa kuwa rais kwa njia ya kidemokrasia na aliiongoza nchi hiyo kwa mara nyingine hadi mwaka 2023.