UhalifuNigeria
Nigeria yafukuza wageni 102 kwa uhalifu wa mtandaoni
21 Agosti 2025Matangazo
Raia mmoja wa Tunisia pia alikuwa miongoni mwa waliorejeshwa makwao huku wageni wengine zaidi wakitarajiwa kufukuzwa kutoka nchini humo katika siku chache zijazo.
Watu hao walikuwa miongoni mwa washukiwa 792 wa uhalifu wa mtandaoni waliokamatwa kufuatia oparesheni iliyofanywa mjini Lagos mnamo Disemba mwaka uliopita.
Nigeria, nchi yenye idadi kubwa ya watu barani Afrika, ina sifa ya kuwa na watu ambao ni matapeli mtandaoni wanaojulikana kwa jina maarufu nchini humo la "Yahoo Boys."
Shirika la EFCC limevamia maficho kadhaa ambapo vijana wahalifu wanajifunza mbinu za utapeli zikiwemo kuwadanganya watu ili kuwatumia pesa ama watoe taarifa muhimu binafsi.
Wahalifu hao mara nyingi huwalenga raia wa Marekani, Canada, Mexico na mataifa ya Ulaya.