Nigeria: Marekani inashinikiza Afrika kuwakubali Wavenezuela
11 Julai 2025Nchi hiyo yenye idadi kubwa kabisa ya watu barani Afrika hata hivyo imesema haiwezi kuwahifadhi wahamiaji hao kutokana na matatizo yake yenyewe.
Serikali ya Rais Donald Trump wiki hii iliwaombamarais watano wa Kiafrika waliozuru Ikulu ya White House kuwachukua wahamiaji kutoka nchi nyingine watakapofukuzwa na Marekani. Waziri Tuggar ameiambia televisheni moja ya nchini Nigeria kuwa Nigeria haiwezi kukubali ombi hilo.
Akizungumza akiwa Brazil alikohudhuria mkutano wa BRICS, Tuggar alisema itakuwa vigumu kwa nchi kama Nigeria kuwachukua wafungwa wa Venezuela. Trump wiki hii aliwakaribisha marais wa Liberia, Senegal, Guinea-Bissau, Mauritania na Gabon katika Ikulu ya White House. Kulingana na afisa wa Marekani na Liberia, aliwasilisha mpango wa nchi za Afrika kuwachukua wahamiaji kutoka nchi nyingine wakati wanafukuzwa na Marekani.