Niger kutaifisha hisa za kampuni ya Urani ya Ufaransa
20 Juni 2025Kampuni hiyo inamiliki asilimia 63 ya hisa za kampuni kubwa ya Somair ya kuchimba madini ya urani nchini Niger. Kampuni hiyo ya Orano imekuwa inaendesha shughuli za migodi ya urani kwa muda wa miongo mitatu nchini Niger.
Hata hivyo, shughuli zake zilifungwa kwenye migodi mitatu muhimu mwaka uliopita baada ya wanajeshi kutwaa madaraka nchini humo. Kampuni hiyo ya Ufaransa imeanza kuchukua hatua za kisheria. Katika tamko lake, serikali ya Niger imesema imepitisha uamuzi huo kutokana na tabia ya kutowajibika na pia kwenda kinyume cha sheria ya kampuni hiyo ya Somair inayomilikiwa na Ufaransa.
Uamuzi huo wa serikali ya Niger unaashiria kuongezeka kwa mzozo kati ya Niger na Ufaransa, kutokana na kuzorota kwa uhusiano kati ya mataifa hayo mawili baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika mwezi Julai mwaka 2023.