NICOSIA:Umoja wa Mataifa yatafakari kurudisha wafanyakazi Iraq
14 Novemba 2003Matangazo
Afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesema leo hii ni vigumu kufikiria kurudishwa kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq venginevyo hali ya usalama nchini humo inaboreka. Kevin Kennedy mkuu wa Tawi la Masuala ya Dharura ya Kibinaadamu ya Ofisi Uratibu wa Masuala ya Kibininaadamu ya Umoja wa Mataifa na maafisa wengine waandamizi wa Umoja wa Mataifa wanakutana nchini Cyprus kuandaa mapendekezo kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan juu ya kurudishwa tena kwa wafanyakazi wa chombo hicho nchini Iraq.Karibu wafanyakazi wote wa Umoja wa Mataifa waliondolewa nchini Iraq kufuatia shambulio la Augusti 19 kwa makao makuu ya umoja huo mjini Baghdad lililopelekea kuuwawa kwa wafanyakazi wake 22 pamoja na wageni akiwemo mkuu wa oporesheni za Umoja wa Mataifa nchini humo Sergio Viera de Melo. Majadiliano yao yanatazamiwa kukamilika mwishoni mwa juma wakati mapendekezo yatakapotolewa kwa Annan.