NICOSIA:Mateka mmoja wa Cyprus bado azuiliwa na waasi Iraq
17 Septemba 2005Matangazo
Serikali ya Cyprus inafanya mazungumzo ya kutaka kuachiliwa huru kwa mfanyibiashara mmoja aliyetekwa nyara wiki moja iliyopita mjini Badhdad.
Karapet Jikerjian ana uraia wa nchi mbili, Cyprus na Lebanon.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Cyprus imetaka usaidizi wa serikali ya Ugiriki na Uingereza ambayo inauongoza Umoja wa Ulaya kwa kuwa Cyprus haina uhusiano wa kidiplomasia na Iraq.
Wateka nyara hao mwanzoni walitaka kiasi cha dola elfu 20 ili kumwacha huru Jikerjian. Kulingana na taarifa iliyotolewa leo na jamaa ya mateka huyo, kundi hilo liliongeza kiasi cha pesa lilizotaka awali kuwa dola milioni mbili mara baada ya mwajiri wake kulipa fedha hizo dola elfu 20.