NEW YORK:UN yataka ielezwe dhima yake Iraq
19 Desemba 2003Matangazo
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan anataka wahusika wakuu wa suala la Iraq kukutana hapo Januari 15 na kuamuwa hasa dhima gani wanayotaka Umoja wa Mataifa itimize wakati nchi hiyo ikielekea katika hatua ya kuondokana na kukaliwa kwa mabavu na Marekani na kuanzisha serikali ilioachaguliwa kidemokrasia.
Akionekana kuvunjika moyo kutokana na kutopatiwa majibu ya ufasaha kutoka kwa Baraza la Utawala nchini Iraq au muungano wa majeshi yanayoongozwa na Marekani nchini humo Annan hapo jana amesema wakati umefika kwa yeye kukaa pamoja na wawakilishi kutoka pande hizo mbili kuzungumzia kile wanachokitaka kutoka kwa Umoja wa Mataifa.
Annan amesema mazungumzo hayo yatakuwa ya pande tatu na ya kutaka yakinisho ili Umoja wa Mataifa uweze kuamuwa iwapo unaweza kutimiza dhima wanayoitaka na kama ndio kwa njia gani na wapi na katika mazingira gani.