NEW YORK:Ripoti ya mpango wa mafuta kwa chakula nchini Iraq.
8 Septemba 2005Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan,amesema matokeo ya ripoti ya tume huru iliyochunguza kashfa inayouhusisha Umoja wa Mataifa na mpango wa mafuta kwa chakula kwa Iraq,imekuwa ni fedheha kubwa kwa wote waliohusika.
Mkuu wa zamani wa hazina wa Marekani,Paul Volcker,ambaye alikuwa mwenyekiti wa tume hiyo na ndie aliyetoa ripoti hiyo,amemshutumu Bwana Annan kama Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,kwa kufanya makosa aliyoyaita ya kiutawala.
Ripoti ya tume hiyo imeendelea kueleza kuwa wale wote waliokuwa wakisimamia mpango huo,walikuwa wakipuuza muelekeo dhahiri wa kuwepo vitendo vya rushwa na ubadhirifu.
Lakini hata hivyo Bwana Volcker amemsafisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan,kuwa hakuhusika kufanya jambo lolote baya katika mpango huo.
Ripoti hiyo pia imeshauri kuna haja kwa Umoja wa Mataifa kufanyiwa mageuzi.