NEW-YORK:Mataifa yenye nguvu yajadili suala la Iran
20 Septemba 2006Matangazo
Mataifa yenye nguvu duniani yamekuwa na majadiliano jana jioni juu ya mpango wa Nuklia wa Iran huku Washington ikitoa mwito wa kuchukuliwa hatua kali dhidi ya Iran baada ya nchi hiyo kushindwa kukomesha shughuli zake za kinuklia kufikia tarehe ya mwisho iliyokuwa imewekwa na Umoja wa mataifa ya Agosti 31.
Majadiliano hayo yalifanyika wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice.
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la Umoja wa mataifa,China,Urussi,Uingereza,Ufaransa na Marekani pamoja na Itali na Ujerumani walihudhuria mkutano huo.
Bibi Rice amesema kwamba atatia kishindo ili nchi zote husika kuunga mkono wito wa Marekani wa kuiwekea vikwazo Iran.