NEW YORK;Baraza La Usalama pia limeilaani kauli ya rais wa Iran
29 Oktoba 2005Matangazo
Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa pia limeelani kauli iliyotolewa na rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad juu ya kutaka kuangamizwa kwa Israel.
Tamko la Baraza La Usalama kulaani kauli hiyo linafuatia msimamo wa katibu Mkuu Kofi Annan wa kuikazia macho Iran na kuikumbusha juu ya wajibu wake wa kimataifa.Wanachama wote 15 wa Baraza La Usalama walikubaliana juu ya tamko hilo.
Wizara ya mambo ya nje ya Iran imesema haikubaliani na tamko hilo .
Wizara hiyo imeuliza katika tamko ililotoa leo kwa nini Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halikulaani vitisho vya Marekani juu ya kuishambulia Iran.Iran pia imesema katika tamko lake kwamba haina nia ya kuishambulia Israel.
.