NEW YORK: Waziri mkuu mpya wa China Wen Jiabao amewasili Marekani
8 Desemba 2003Matangazo
kwa ziara ya siku 4. Akiwasili mjini New York, alitamka ziara yake itachangia utanuzi wa mahusiano ya busara kati ya nchi mbili. Anatagemewa kupokelewa na rais George W Bush Jumaane, hiyo kesho. Kuna masuala kadhaa yazushayo mvutano kati ya Marekani na China, kama kwa mfano suala la Taiwan. China inataka kuungwa mkono msimamo wake, kwani inakiangalia kisiwa Taiwan kama mkoa wake ulioasi. Mada nyingine itakuwa ni mauzo ya bei rahisi ya China nchini Marekani. Karibuni serikali ya Marekani ilitangaza ushuru wa hali ya juu kwa baadhi ya vitambaa na zana za Televizeheni kutoka China.