New York: Russia yatuhumu mipango ya Marekani nchini Iraq
20 Novemba 2003Marekani na Uingereza zikijitafutia uungaji mkono wa ajenda yao ya kukabidhiwa madaraka Wairaki, Russia hiyo jana ilikosoa mipango ya Marekani kutoujumuisha zaidi Umoja wa Mataifa katika utaratibu wa mpito. Halmashauri tawala ya wanachama 25 nchini Iraq, inatazamiwa kutoa ratiba mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hadi tarehe 15 Disemba, juu ya kukabidhiwa madaraka na muungano unaoongozwa na Marekani hadi tarehe 13 Juni, mwaka 2004, ingawa ratiba hiyo ingetolelwa mapema zaidi.Lakini waziri wa mambo ya nje wa Russia, Igor Ivanov, aliiambia televisheni ya CNN, kwamba mapendekezo hayakufichua wazi wazi jukumu la Umoja wa Mataifa, ambalo Russia, Ufaransa na Ujerumani zimesema lazima lijipatie umuhimu mkubwa katika ufumbuzi wowote ule.