NEW YORK: Mswada wa azimio kuhusu Iran wakubaliwa
29 Julai 2006Matangazo
Wanachama 5 wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Ujerumani,wamekubaliana na mswada wa azimio unaohusika na mgogoro wa kinuklia wa Iran.Mswada huo unaotazamiwa kupitishwa mapema juma lijalo,utaipa Iran muda hadi mwisho wa mwezi Agosti,kusita kurutubisha madini ya uranium na vile vile kutekeleza masharti yote ya shirika la kimataifa la nishati ya kinuklia.Isipofanya hivyo kuna kitisho cha kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia. Urussi na China lakini zimeshinikiza kuwa kwa hivi sasa Iran isiwekewe vikwazo bali ionywe tu.