New-York: Katika juhudi za kusimamia mzozo wa Iraq katibu mkuu wa...
27 Novemba 2003Matangazo
Umoja wa mataifa Kofi Annan anapanga kuunda tume maalum ya mashauriano.Tume hiyo yenye wanachama 16,inajumuisha mataifa sita jirani na Iraq pamoja na Misri,wanachama watano wa kudumu wa baraza la usalama na wanachama wengine kadhaa wa muda,ikiwemo pia Ujerumani.Tume hiyo imeundwa kumsaidia katibu mkuu Kofi Annan katika kusimamia shughuli za umoja wa mataifa nchini Iraq.Duru ya kwanza ya mazungumzo kati ya katibu mkuu wa Umoja wa mataifa na wawakilishi wa nchi zinazounda tume hiyo ya mashauriano,imepangwa kuitishwa jumatatu ijayo.Ujerumani,Ufaransa na Rashia zinatetea umuhimu wa kuwajibika ipasavyo Umoja wa mataifa katika ujenzi mpya wa Iraq.