New York. Katibu mkuu ahiirisha ziara ya Iran.
5 Novemba 2005Matangazo
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Kofi Annan amefuta ziara yake nchini Iran.
Hii inakuja baada ya rais wa Iran kusema kuwa Israel inapaswa kufutwa kutoka katika ramani ya dunia.
Annan alipanga kufanya ziara mjini Tehran katikati ya mwezi Novemba.
Mjini Tehran , msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni amesema kuwa ilikuwa ni Iran na sio Annan aliyehitaji ziara hiyo ibadilishwe ili kuangukia katika muda mzuri zaidi hapo baadaye.